Category: Nukuu za Prof. Ngowi

0

“WALIMU, MAPROFESA TUTOKE MAOFISINI, TUKATAFITI ILI TUJUE MAHITAJI YA SOKO” Prof. NGOWI

Mmbobezi wa Uchumi Prof.Ngowi akihojiwa na vyombo vya habari juu ya mustakabali wa elimu Nchini, asema kuna haja ya wasomi, walimu na Maprofessor, kutoka katika ofisi zao na kwenda kufanya tafiti ili kujua waajiri, waajiriwa na wanaojiajiri wenyewe wanahitaji nini na kisha wawaandae vijana kulingana na mahitaji ya soko. Lakini pia umuhimu wa kuwafundisha vijana kuwa na moyo wa kuipenda Nchi yao na kutumia rasimali za Nchi yao vizuri na kuachana na mawazo ya kuiba na kujipatia utajiri wa haraka haraka

0

MUDA MZURI WA KUJINDAA KUSTAAFU

Unafahamu ni muda gani sahihi wa kujiandaa kabla ya kustaafu? Je ni maandalizi gani unapaswa kufanya ili unapostaafu uishi maisha yasiyo na usumbufu wa aina yeyote? Prof Ngowi ana ushauri mzuri kwa ajili yako.

0

USIKUBALI KUZAMA NA BIASHARA YAKO

Kama mjasiriamali, usikubali kuzama/kuangamia na biashara yako. Lazima uwe mjanja kwa kutafuta suluhisho la changamoto unazokumbana nazo kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. Jifunze kutoka kwa wenye uzoefu pia, ni vipi wao walikwepa ama kukabiliana na tatizo unalokumbana nalo.

0

SERIKALI NA SOKO HURIA

Mwingiliano huru wa nguvu za Ugavi na utashi katika soko huru ni muhimu, hata hivyo inaweza kuwa muhimu zaidi kwa serikali kuingilia kati kurekebisha hali pale soko linaposhindwa kuweka mambo sawa.

0

MKONO WA SHUKRANI

Unapofanya kazi/biashara na ikaleta matunda ni lazima kukumbuka kurudisha sehemu ya faida kwa jamii. Iwe kwa njia yeyote ile, jitahidi kuihudumia jamii kwa moyo mkunjufu.