Category: Nje Ya Box

0

TGNP YASISITIZA BAJETI 2019/2020 IWE YA MLENGO WA JINSIA NA JUMUISHI

Wadau kutoka katika sekta mbalimbali nchini wakiwemo wanazuoni, wanaharakati, wawakilishi wa Serikali, , washirika wa maendeleo, waungana na TGNP mtandao kusisitiza umuhimu wa bajeti ya mwaka 2019/2020 kuwa bajeti ya mlengo wa jinsia na iliyo jumuishi . Hayo yamesemwa katika mjadala kabla ya bajeti kuu 2019/2020 ulioratibiwa na TGNP Mtandao mnamo tarehe 2 April 2019 katika Hoteli ya New Africa Dar es Salaam

0

“NILIANZA NA KUKU 13 TU, SASA HIVI NINA TENGENEZA MILIONI MBILI KILA WIKI”

Makala ya mjasiriamali inayoonyesha jinsi mjasiriamali alivyotajirika kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji. Kuku wa kienjeyi wamekuwa chanzo cha mapato kwa kaya nyingi hapa nchini. Lakini kuna watu wameamua kuchukulia ufugaji wa kuku kama kazi yao ya kila siku, na matunda wanayaona. Mfano mzuri ni mjasiriamali huyu ambaye alianza na kuku 13 na sasa anaingiza takribani shilingi milioni mbili kila wiki. Je amefanyaje kufika hapa? Amekutana na vikwazi gani? Msikilize

0

“WALIMU, MAPROFESA TUTOKE MAOFISINI, TUKATAFITI ILI TUJUE MAHITAJI YA SOKO” Prof. NGOWI

Mmbobezi wa Uchumi Prof.Ngowi akihojiwa na vyombo vya habari juu ya mustakabali wa elimu Nchini, asema kuna haja ya wasomi, walimu na Maprofessor, kutoka katika ofisi zao na kwenda kufanya tafiti ili kujua waajiri, waajiriwa na wanaojiajiri wenyewe wanahitaji nini na kisha wawaandae vijana kulingana na mahitaji ya soko. Lakini pia umuhimu wa kuwafundisha vijana kuwa na moyo wa kuipenda Nchi yao na kutumia rasimali za Nchi yao vizuri na kuachana na mawazo ya kuiba na kujipatia utajiri wa haraka haraka

0

NJE YA BOX – EPISODE 9

Kuna ujumbe hapa, mzuri kabisa “Hauwezi kuondokana na umasikini kwa kulala tu, ni lazima upambane na ugangamale.” Wengi tunapenda kulala na kuendekeza uvivu, kitu ambacho tunashauriwa kuachana nacho ili kupata maendeleo. Kama hutaamka na kufanya kazi, basi usitegemee maendeleo!

0

NJE YA BOX – EPISODE 8

“Kama ukiendelea kukaa vijiweni na kupiga kelele juu ya tatizo la umasikini linalokukabili basi utabaki kuwa mpiga filimbi tu na kamwe hautatoka.” Ni maneno ya Ibrahimu Juma. Yeye anaamini katika kufanya kazi zaidi ya kuongea na kulalamika kila mara. Na yuko sahihi kabisa, angalia video hii upate ujumbe kisha uutendee kazi.

0

NJE YA BOX – EPISODE 7

Ndesambuka Merinyo anakuambia kwamba “Kipaji chako ni tunu kutoka kwa mwenyezi Mungu, Kipaji chako ni Chimbo la dhahabu” Je ni wangapi huwa wanagundua vipaji vyao na kuvitumia katika kujiendeleza ama kujiletea maendeleo? Kama bado hujaanza kutumia kipaji chako, anza sasa.