Category: Mjasiriamali

0

UTAMU WA PILIPILI YA VIVA PLUS, WAIFANYA IWE GUMZO NDANI NA NJE YA NCHI

Mjasiriamali Mc Luciana, mkurugenzi wa kampuni ya Viva Plus , ambao ndiyo wazalishaji wa Pilipili ya Viva Plus, athibitisha kwamba wajasiriamali watanzania wakiamua basi wanaweza. Pilipili hii ambayo hutengenezwa na vitu asilia vinavyolimwa na wakulima wa hapa nchini imeonekana kuteka soko la ndani na nje ya nchi. Kama mjasiriamali tafadhali tazama makala haya na ujionee ni nini hasa maana ya ubunifu.

0

WAZALISHAJI WADOGO WA BIDHAA ZA NGOZI WAFAIDIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA MZUMBE

Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam, kwa kushirikiana na Benki ya NMB tawi la Ilala, wametoa mafunzo ya ujasiriamali kwa Wazalishaji wadogo wa bidhaa za ngozi katika soko la wamachinga , Machinga Complex jijini Dar es Salaam. Wajasiriamali hawa wamejifunza mambo mengi ikiwemo jinsi ya kusajili biashara zao, jinsi ya kutunza hesabu, matumizi sahihi ya benki na mitandao katika biashara na kadhalika. Team nzima ya NgowiTV ilikuwepo kuhakikisha kuwa mafunzo yanaenda vizuri, na mafunzo haya yaliratibiwa na wananfunzi wa Mzumbe kutoka kampasi ya Dar es salaam kwa udhamini wa benki ya NMB.

0

MPANGO WA BIASHARA NI MUHIMU KWA UFANISI WA BIASHARA YAKO”Prof. Ngowi

Prof. Ngowi awafundisha Wajasiriamali wadogo wadogo kutoka mkoani Dar Es Salaam, juu ya umuhimu wa wa kuwa na Mpango wa Biashara katika biashara zao, mambo muhimu yanaopaswa kuwepo katika andiko hilo la Mpango wa Biashara, katika semina maalumu ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo iliyoratibiwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa kushirikiana na Taasisi ya KUHNE FOUNDATION ya Ujerumani, iliyofanyika kuanzia tar 23-25 April 2019, Chuo kikuu cha mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam

0

“NILIANZA NA KUKU 13 TU, SASA HIVI NINA TENGENEZA MILIONI MBILI KILA WIKI”

Makala ya mjasiriamali inayoonyesha jinsi mjasiriamali alivyotajirika kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji. Kuku wa kienjeyi wamekuwa chanzo cha mapato kwa kaya nyingi hapa nchini. Lakini kuna watu wameamua kuchukulia ufugaji wa kuku kama kazi yao ya kila siku, na matunda wanayaona. Mfano mzuri ni mjasiriamali huyu ambaye alianza na kuku 13 na sasa anaingiza takribani shilingi milioni mbili kila wiki. Je amefanyaje kufika hapa? Amekutana na vikwazi gani? Msikilize

0

“INAWEZEKANA KWA WAZAWA KUWEKEZA KWENYE SEKTA MUHIMU ZA KIUCHUMI”Waziri Mkuu Kasim Majaliwa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kasim Majariwa, amesema Serikali inafarijika sana pale inapoona Mzawa anafanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta muhimu ambazo ni mhimiri katika uchumi wa nchi. Waziri mkuu ameyasema hayo mnamo tarehe 28 novemba 2018 alipotembelea mradi mpya wa kisasa wa kuchenjulia dhahabu unaojengwa na kampuni ya uchenjuaji dhahabu ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd, iliyopo mkoani Geita inayomilikiwa na mzawa Hussein Nassor Amar ,

0

KUPATA ALAMA MOJA TU KWA PROF. NGOWI SHURTI UGANGAMALE KWELI!

Prof. Ngowi akimsikiliza mwanafunzi wake wa MBA Corporate Management, Jonathan Nkwabi, alipompa dakika kadhaa za kuwakilisha Darasa lake na kuelezea mradi wa masomo kwa vitendo unaondelea hivi sasa chuoni Mzumbe, katika kongamano la kambi ya ujasiriamali lililofanyika hivi karibuni Mzumbe Morogoro. Prof. Ngowi aliridhishwa kwa kiasi kikubwa na uwasilishaji wa mwanafunzi wake huyo na kumpa alama moja kati ya 20. Kupata alama moja shurtí ugangamale lakini mkitoka hapo mtatusaidia kulipeleka Taifa hili kwenye Uchumi wa kati.

“HII NIMOJA KATI YA MBINU MPYA YA KUFUNDISHA WANAFUNZI KWA VITENDO HAPA MZUMBE” – Prof Ngowi 0

“HII NIMOJA KATI YA MBINU MPYA YA KUFUNDISHA WANAFUNZI KWA VITENDO HAPA MZUMBE” – Prof Ngowi

Prof, Honest P. Ngowi(PhD ECONOMICS) kutoka chuo kikuu cha Mzumbe, akionesha jinsi Chuo Kikuu cha Mzumbe kilivyodhamiria kwa vitendo kwa kuja na mbinu mbadala za ufundishaji wanafunzi wake kwa vitendo zaidi, katika Kongamano la Kambi ya Ujasiriamali iliyofanyika 17/05/2015, Chuo Kikuu Mzumbe.