Category: Clinic ya UJASIRIAMALI

0

UTAMU WA PILIPILI YA VIVA PLUS, WAIFANYA IWE GUMZO NDANI NA NJE YA NCHI

Mjasiriamali Mc Luciana, mkurugenzi wa kampuni ya Viva Plus , ambao ndiyo wazalishaji wa Pilipili ya Viva Plus, athibitisha kwamba wajasiriamali watanzania wakiamua basi wanaweza. Pilipili hii ambayo hutengenezwa na vitu asilia vinavyolimwa na wakulima wa hapa nchini imeonekana kuteka soko la ndani na nje ya nchi. Kama mjasiriamali tafadhali tazama makala haya na ujionee ni nini hasa maana ya ubunifu.

0

WAZALISHAJI WADOGO WA BIDHAA ZA NGOZI WAFAIDIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA MZUMBE

Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam, kwa kushirikiana na Benki ya NMB tawi la Ilala, wametoa mafunzo ya ujasiriamali kwa Wazalishaji wadogo wa bidhaa za ngozi katika soko la wamachinga , Machinga Complex jijini Dar es Salaam. Wajasiriamali hawa wamejifunza mambo mengi ikiwemo jinsi ya kusajili biashara zao, jinsi ya kutunza hesabu, matumizi sahihi ya benki na mitandao katika biashara na kadhalika. Team nzima ya NgowiTV ilikuwepo kuhakikisha kuwa mafunzo yanaenda vizuri, na mafunzo haya yaliratibiwa na wananfunzi wa Mzumbe kutoka kampasi ya Dar es salaam kwa udhamini wa benki ya NMB.

0

MPANGO WA BIASHARA NI MUHIMU KWA UFANISI WA BIASHARA YAKO”Prof. Ngowi

Prof. Ngowi awafundisha Wajasiriamali wadogo wadogo kutoka mkoani Dar Es Salaam, juu ya umuhimu wa wa kuwa na Mpango wa Biashara katika biashara zao, mambo muhimu yanaopaswa kuwepo katika andiko hilo la Mpango wa Biashara, katika semina maalumu ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo iliyoratibiwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa kushirikiana na Taasisi ya KUHNE FOUNDATION ya Ujerumani, iliyofanyika kuanzia tar 23-25 April 2019, Chuo kikuu cha mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam

“WAJASIRIAMALI NI LAZIMA MJUE KUTOFAUTISHA IPI NI GHARAMA NA IPI NI FAIDA ” Prof. Ngowi 0

“WAJASIRIAMALI NI LAZIMA MJUE KUTOFAUTISHA IPI NI GHARAMA NA IPI NI FAIDA ” Prof. Ngowi

Prof. Ngowi awafunda wajasiriamali nchini kuhakikisha wanajua kukotoa mahesabu vyema(bajeti) na kujua jinsi ya kutofautisha kati ya gharama na faida ili waweze kupata faida stahiki na kupata maendeleo. ametoa darasa hilo alipomtembelea mjasiriamali Festo Nyoni ambaye ni fundi seremala aliyejiajiri mwenyewe, katika kipindi chake cha Clinic ya Ujasiriamali