About

NGOWI TV ni kituo cha televisheni katika mtandao (online television) kinachojikita katika kutoa elimu na habari zilizochambuliwa kuhusu masuala ya uchumi, biashara na maendeleo duniani na Tanzania. Inafanya chambuzi za kisayansi za mambo ya uchumi na biashara na jinsi mambo haya yanahusiana na maendeleo katika ujumla wake. Inalenga kuwa kituo mahiri katika kuelimisha, kuarifu na kushauri jamii na wafanya maamuzi kuhusu uchumi, biashara na maendeleo katika mapana yake.